
Mwanamuziki maarufu duniani Shakira amethibitisha kuachana na Gerard Piqué baada ya miaka 11 ya kuwa kwenye mahusiano.
Timu yake ya mawasiliano imetoa taarifa rasmi kupitia mtandao wa Twitter ambapo imeandika “Tunasikitika kuthibitisha kwamba tumeachana rasmi. Kwa ustawi wa watoto wetu, ambao ndio kipaumbele chetu kikubwa zaidi, tunakuomba kwamba uheshimu faragha yao. Asante.”
Sababu kuu iliyopelekea wawili hawa kuachana ni tuhuma za usaliti ambapo inadaiwa Shakira alimfumania Gerard Piqué akiwa na mwanamke mwingine.
Utakumbuka kwa pamoja wamebarikiwa kupata watoto wawili wa Kiume.