Entertainment

PENZI LA SHAKIRA NA PIQUE LAINGIWA NA UKUNGU

PENZI LA SHAKIRA NA PIQUE LAINGIWA NA UKUNGU

Mwanamuziki maarufu duniani Shakira anadaiwa kumfumania mumewe mchezaji staa wa Barcelona Gerard Piqué akiwa na mwanamke mwingine, hiyo imepelekea wawili hao kwa sasa kila mmoja kuishi kivyake huku penzi lao likiwa mbioni kuvunjika. Kwa mujibu wa Mwandishi wa Gazeti la El Periodico, Emilio Pérez de Rozas.

Shakira na Pique walianza mahusiano mwaka 2011 baada ya kukutana kwenye video ya “Waka Waka (This Time for Africa)” mwaka 2010. Pamoja wana watoto wawili wa Kiume. Jarida la Forbes linawataja Shakira na Pique kwenye orodha yao ya Couples zenye nguvu zaidi duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *