
Msanii Weezdom hatimaye amethibitisha kuwa yeye na mpenzi wake wa siku nyingi Mylee Staicey sio wapenzi tena.
Katika kikao cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram, shabiki mmoja alimuuliza msanii huyo kama bado ni wapenzi na Mylee Staicey na ndipo alipoweka wazi kuwa waliachana zamani.
Kutokana na hilo kama ulikuwa unadhani penzi la weezdom na Stacey lilikuwa limefufuka miezi miwili iliyopita nikuambie tu pole kwani ni wazi kuwa penzi lao limeingiwa na ukungu.
Hata hivyo, bado haijebainika kama kuna ukweli wowote kuhusu stori za wawili hao kuachana ila jambo la kusubiriwa.
Itakumbukwa taarifa za wawili hao kuachana zilianza kusambaa mitandaoni mwaka wa 2020 ambapo ilidaiwa kuwa weezdom na mchumba wake stacey wamevunja penzi lao kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutoaminiana