LifeStyle

Peter Miracle Baby Afichua Ukweli Kuhusu Mtoto wa Shalkido

Peter Miracle Baby Afichua Ukweli Kuhusu Mtoto wa Shalkido

Mwanamuziki Peter Miracle Baby, memba wa kundi la Sailors, amepuuzilia mbali madai kuwa marehemu Shalkido aliacha mtoto, akisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli.

Akizungumza kwenye mitandao ya kijamii, Miracle Baby ameonekana kukerwa na kitendo cha mwanamke mmoja kujitokeza mtandaoni na kudai alizaa mtoto na Shalkido, akisema madai ya mwanamke huyo hayana msingi wowote kwani anatumia jina la marehemu kutafuta kiki wakati familia bado ipo kwenye majonzi.

Miracle Baby amesema kuwa kama kweli Shalkido angepata mtoto, basi bibi yao (Grandmother) angekuwa anafahamu hilo kwa sababu marehemu alikuwa karibu sana na familia yake.

Pia amekiri kuwa Shalkido alikuwa na mpenzi enzi za uhai wake lakini walitengana muda mrefu kabla ya kifo chake, na hawakuwahi kupata mtoto kutokana na hali ngumu ya maisha waliyokuwa nayo wakati huo.

Katika hatua nyingine amenyosha maelezo kuhusu picha inayoenea mtandao ikimuonyesha Shalkido akiwa na mtoto mchanga, akisema mtoto huyo si wake, bali ni wa dada yake ambaye alilelewa na bibi yao (Grandmother).

Hata hivyo, amewataka walimwengu kuacha kueneza uvumi usio na msingi na kumruhusu Shalkido kupumzika kwa amani, akisisitiza kuwa kutumia jina la marehemu kwa kiki ni kukosa heshima kwa familia na marafiki waliobaki.

Ibada ya wafu ya kumuaga msanii Shalkidoh inatarajiwa kufanyika leo katika kanisa la All Saints Cathedral, Nairobi, kuanzia saa 11:30 asubuhi. Ibada hiyo inatarajiwa kuwaleta pamoja wasanii, wadau wa muziki, na mashabiki wengi watakaoungana kumuaga Shalkido kwa heshima na upendo kabla ya mazishi yake Alhamisi Oktoba 16.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *