Msanii chipukizi kutoka Tanzania, Pipi Jojo, amegusa hisia za mashabiki baada ya kufichua kwamba hajawahi kupata upendo wa baba kama anaoupata sasa kutoka kwa Chief Godlove, ambaye amekuwa akionyesha wazi kujivunia kumlea kama mwanawe.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Pipi Jojo ameeleza kuwa katika maisha yake yote tangu kuzaliwa, hakuwahi kutegemea kama siku moja angepata nafasi ya kufurahia mapenzi ya baba.
Msanii huyo, amesema kwamba hatua ya Chief Godlove kumpa nafasi kama binti yake imekuwa moja ya baraka kubwa maishani mwake, na kwamba anathamini sana uhusiano huo mpya.
Binti huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 16, ameeleza kuwa anafurahia kupendwa na kutunzwa kama binti halisi, na kwamba hatamuangusha mtu ambaye amempa nafasi ambayo kwa muda mrefu hakuwahi kuipata.