Sports news

Police Bullets Yaweka Rekodi Kundi A CECAFA

Police Bullets Yaweka Rekodi Kundi A CECAFA

Police Bullets FC imeanza vyema kampeni ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, baada ya kuichapa Kampala Queens bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyayo. Bao hilo la ushindi lilifungwa na Emily Moranga mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Police sasa itamenyana na DenDen FC ya Eritrea katika mechi yao ya pili na ya mwisho ya makundi.

Katika matokeo mengine, mabingwa watetezi CBE kutoka Ethiopia walilazwa 2-1 na Rayon Sports ya Rwanda. Michuano ya Kundi C inatarajiwa kuanza kesho kwa pambano kati ya JKT Queens na JKU Princess.

Timu zitakazoshika nafasi ya kwanza kila kundi na moja ya pili yenye alama nyingi zitafuzu nusu fainali zitakazopigwa Septemba 14, huku fainali ikifanyika Septemba 16. Bingwa atawakilisha CECAFA kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *