Police Bullets Yaweka Rekodi Kundi A CECAFA

Police Bullets Yaweka Rekodi Kundi A CECAFA

Police Bullets FC imeanza vyema kampeni ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, baada ya kuichapa Kampala Queens bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyayo. Bao hilo la ushindi lilifungwa na Emily Moranga mwanzoni mwa kipindi cha pili. Police sasa itamenyana na DenDen FC ya Eritrea katika mechi yao ya pili na ya mwisho ya makundi. Katika matokeo mengine, mabingwa watetezi CBE kutoka Ethiopia walilazwa 2-1 na Rayon Sports ya Rwanda. Michuano ya Kundi C inatarajiwa kuanza kesho kwa pambano kati ya JKT Queens na JKU Princess. Timu zitakazoshika nafasi ya kwanza kila kundi na moja ya pili yenye alama nyingi zitafuzu nusu fainali zitakazopigwa Septemba 14, huku fainali ikifanyika Septemba 16. Bingwa atawakilisha CECAFA kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake.

Read More
 Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa Ligi Kuu ya soka FKF yapata pigo

Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa Ligi Kuu ya soka FKF yapata pigo

Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini FKF yalipata pigo baada ya kutoka sare na Sofa Paka bao moja kwa moja katika mechi iliyochezwa uwanjani Kenyatta, mjini Machakos. Donata Okello aliipa Sofa Paka bao la uongozi dakika 37 na kulazimisha matokeo hayo kufikia wakati wa mapumziko. Hata hivyo katika kipindi cha pili Brian Okoth aliisawazishia polisi katika dakika ya 87 huku mechi hiyo ikamalizika kwa sare ya goli moja kwa moja. Kwenye mechi zingine zilizochezwa leo Bandari FC ilipata ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Muranga Seal, Shabana FC na Kariobangi Sharks zikatoka sare tasa, FC Leorpards iliilaza Nairobi City Stars bao moja kwa nunge nayo Tusker FC ikatoka sare kapa na KCB.

Read More