Gossip

Polisi Uganda Wakanusha Kumkamata Alien Skin

Polisi Uganda Wakanusha Kumkamata Alien Skin

Polisi nchini Uganda wamekanusha taarifa zilizodai kwamba msanii mwenye utata Alien Skin amekamatwa kwa tuhuma za mauaji.

Kupitia msemaji wa Polisi wa Kanda ya Kampala, imeelezwa kwamba msanii huyo hajakamatwa na hayupo mikononi mwao, lakini anasakwa na vyombo vya dola.

Polisi wamewataka wananchi kutoa taarifa iwapo kuna mtu yeyote anayefahamu alipo, kwa kuwa msanii huyo yupo kwenye orodha ya wahalifu wanaotafutwa.

Kauli ya Polisi inakuja siku chache baada ya mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii kusambaza taarifa kwamba bosi huyo wa Fangone Forest amekamatwa na kutupwa rumande kwa makosa mbalimbali ikiwemo mauji ya dansa maarufu wa Kampala, ambaye alizikwa wiki iliyopita katika Wilaya ya Mbale.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *