
Rapa wa Kenya Prezzo amefunguka mara ya kwanza baada ya kupoteza kiti cha ubunge eneo la kasarani kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika juzi kati.
Katika mahojiano Prezzo amesema ingawa hakubahatika kushinda kiti cha bunge Kasarani ataendelea kuwafanyia kazi wananchi huku akijitayarisha kuwania tena kiti hicho mwaka wa 2027.
Hitmaker huyo wa “Mafans” amesema hajawahi poteza kitu chochote anachokitamani katika maisha yake na hatua ya kushindwa kwenye kinyanganyiro cha ubunge kasarani kwenye uchaguzi mkuu nchini kenya ni anguko lake la kwanza maisha.
Hata hivyo anaamini kushindwa kwake kwenye ubunge kasarani ilitokana na yeye kutotoa pesa ikilinganishwa na wapinzani wake ambao walikuwa wanawahonga wananchi ili wawape kura