
Rapa Prezzo amewachana wasanii nchini Kenya wanaodanganya kuhusu miaka yao halisi ya kuzaliwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram ameshangazwa na kasumba hiyo ambayo imekithiri sana miongoni mwa mastaa nchini huku akisema kuwa ni jambo la aibu kwao kuficha umri kwa ajili ya kuwafurahisha walimwengu.
Rapa huyo mkongwe amewataka mastaa hao kuacha kadhi ya kupunguza umri na badala yake wamshukuru mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai.
“It puzzles me when folks are ashamed of their age. I mean instead of giving thanks for the gift of life they try source for a calculator that can deduct their age or something. Shit is trimilising!” Aliandika.