Entertainment

Prodyuza kutoka Tanzania S2kizzy ashirikishwa kwenye Album ya Black Eyed Peas “Elevation”

Prodyuza kutoka Tanzania S2kizzy ashirikishwa kwenye Album ya Black Eyed Peas “Elevation”

Mtayarishaji wa Tanzania S2kizzy ameshiriki kwenye kuitayarisha Album mpya ya Kundi maarufu la Muziki duniani Black Eyed Peas “Elevation” ambayo imetoka rasmi wiki hii. Zombie ameshiriki kutayarisha wimbo namba 9 kwenye Album hiyo uitwao “Filipina Queen” ambao ameshirikishwa mwanadada Bella Poarch.

Kwenye Album hiyo yenye vyuma 15, Black Eyed Peas wamewapa mashavu wakali wa dunia kama Shakira, Ozuna, David Guetta, Daddy Yankee na wengine. Kundi hilo linaundwa na wasanii wanne akiwemo William James Adams Jr, Allan Pineda Lindo (apl.de.ap), Jaime Luis Gomez (Taboo) na J. Rey Soul. Kundi hilo lilifanikiwa kuitikisa dunia na Hit single yao “Where Is The Love” mwaka 2003.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *