Entertainment

Prodyuza Mike Dean atemana na Kanye West kisa sarakasi zake mtandaoni

Prodyuza Mike Dean atemana na Kanye West kisa sarakasi zake mtandaoni

Mtayarishaji na Mkandarasi (Engineer) wa muziki lakini pia rafiki wa muda mrefu wa rapa Kanye West aitwaye Mike Dean ametangaza kutemana na rapa huyo kufuatia mwenendo wake wa kila siku.

Mike Dean ametoa ya moyoni kwa kusema Kanye amejikita kwenye kutafuta attention ya vyombo vya habari kuliko hata maisha yenyewe. Anasema YE amekuwa akifanya upuuzi ambao unapewa nafasi ya kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari kiasi cha kuwanyima nafasi wanaofanya vizuri kisanaa na wanaostahili kuzungumzwa.

Mike Dean amekuwa sehemu ya Kanye West kwenye muziki wake kwa kipindi kirefu akitayarisha Album zake na hata kuhusika kwenye matamasha yake mbali mbali upande wa sound.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *