
Producer Mkongwe wa muziki kutoka nchini Tanzania, P Funk Majani amesema albamu yake imekamilika kwa asilimia 80.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter prodyuza huyo kutoka Bongo Records amesema album itaingia sokoni machi 30 mwaka huu wa 2022 ingawa hajaweka wazi jina la album na idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album yak hiyo.
“My album MAJANI is 80% complete, God willing we Dropping on March 30th 2022!!!” ameandika Majani Twitter.
P Funk Majani anakuja na albamu hiyo mara baada ya mwaka jana kusimamia albamu ya Rapcha, Wanangu 99 iliyotoka na ngoma 10.
Utakumbuka mwaka jana Producer mwingine Tanzania, Marco Chali aliachia albamu yake, iitwayo ONA.