
Promota wa muziki Abtex Musinguzi maarufu kama Abtex amekamatwa na polisi baada ya watu 10 kupoteza maisha kutokana na mkanyagano katika shoo aliyokuwa ameiandaa kwenye ukumbi wa Freedom City mwishoni mwa mwaka 2022.
Mshereheshaji wa shoo hiyo aliwaagiza mashabiki watoke nje ya ukumbi huo na kuelekea kwenye maegesho ya magari kushuhudia mbwembwe za kuukaribisha mwaka mpya 2023.
Kwa haraka, zaidi ya watu 1,000 walijaribu kupita kwenye lango dogo lilokuwa wazi lakini kwa bahati mbaya watu walikanyangana vibaya kwani maeneo mengine ya ukumbi wa Freedom City yalikuwa yamefungwa.
Hata hivyo jeshi la Polisi nchini Uganda linawatafuta waandaaji na mameneja walioandaa shoo hiyo ili kujibu baadhi ya maswali kufuatia sakata la vifo vya mashabiki.