Entertainment

PROMOTA ROBERT MUTIMA AOMBA RADHI KWA SPICE DIANA

PROMOTA ROBERT MUTIMA AOMBA RADHI KWA SPICE DIANA

Promota wa muziki kutoka Uganda Robert Mutima amemuomba msamaha msanii Spice Diana baada ya kushindwa kumlipa pesa zake.

Katika taarifa promota huyo amekiri kumvunjia heshima mrembo huyo kwa kusema kwamba hakuweza kumlipa kwa wakati kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

Hata hivyo Spice Diana amepokea msamaha wa promota huyo kwa mikono miwili huku akisema hana kinyongo naye ila alikuwa anadai haki yake.

Wikiendi iliyopita, mashabiki waliachwa na mshangao baada ya Spice Diana kusimamisha show yake ghafla huko Masaka ambapo alianza kumsomea Robert Mutima akitaka amlipe pesa zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *