Entertainment

R. Kelly akanusha kuhusu kuachia Album mpya

R. Kelly akanusha kuhusu kuachia Album mpya

Mkongwe wa muziki wa RnB kutoka nchini Marekani Robert Sylvester Kelly alimaarufu kama R Kelly ameachia album yake licha ya kuwa gerezani.

Licha ya kuachia Album hiyo ya aliyoipa jina la I ADMIT IT ikiwa na ngoma 13, Kampuni ya Sony Music iliishusha Album hiyo kwenye majukwaa ya Spotify na Apple Music.

Mwanasheria wa Mwanamuziki huyo mkongwe, Jennifer Bonjean amekaririwa na mtandao wa The Hollywood Reporter akisema, Album hiyo ilichiwa bila kuidhinishwa, ni kazi ambayo iliwahi kuibiwa. Bonjean aliendelea kusema kwamba waliwahi kutoa taarifa polisi kwamba kuna baadhi ya ‘Masters’ za R. Kelly ziliwahi kuibiwa lakini hawakufanya uchunguzi wowote.

“Pindi anakamatwa, kulikuwa na vifaa vya studio ambavyo vilichukuliwa. Masters zake zilipotea. Kwa hiyo ni nani aliyekuwa nazo na nani anafaidika nazo, hatumfahamu.” Alisema

Tunafahamu kwa R Kelly yupo gerezani akitumikia kifungo cha miaka 30 kwa makosa mbalimbali ya unyanaysaji Kingono kwa watoto wenye umri mdogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *