Entertainment

R. Kelly na mchumba wake wapata mtoto

R. Kelly na mchumba wake wapata mtoto

Mwimbaji nguli wa RnB, R.Kelly na mchumba wake, bibie Joycelyn Savage wamepata mtoto wao wa kwanza wakike, aliyepewa jina “Ava Lee Kelly”, ambapo wamepata mtoto huyo kwa njia ya upandikizaji.

R.Kelly ambaye kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo chake, mchumba wake huyo amebainisha kujifungua kupitia mfululizo wa post zake katika ukurasa wake wa Instagram pamoja na ku-share picha za kichanga hicho, akieleza kajifungua tarehe 8 mwezi huu.

Hata hivyo, sio R.Kelly wala Wakili wake aliyethibitisha ukweli wa taarifa hiyo ikizingatiwa mrembo Joycelyn Savage (pichani) alikuwa ni miongoni mwa wahanga wa vitendo vya kinyama vya msanii R.Kelly ambapo Julai mwaka huu alijitokeza hadharani na kumtetea mwanamuziki huyo huku akisema kwamba walikuwa wachumba na ana ujauzito wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *