
Wanamuziki nyota kutoka Afrika Kusini Cassper Nyovest na AKA bado wanaendelea kutupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii licha ya kuwahi kuonekana pamoja lakini inawezekana bifu lao halitaishi hivi karibuni.
Leo yameibuka makubwa baada ya Cassper kupitia ukurasa wake wa Twitter, ku-post picha ya AKA akiwa ameshikilia kinywaji chake cha pombe (Billiato) na kumtangaza kama Balozi mpya wa kileo hicho. Tweet hiyo imewashtua wengi na kuanza kuhoji imekuwaje?
Sasa AKA amejibu madai hayo kwa kusema kwamba taarifa zilizotolewa na Cassper Nyovest hazina ukweli wowote na yupo mbioni kumfungulia mashtaka kwa kumharibia haki zake kibiashara hasa kipindi hiki ambacho anafanya kazi na makampuni mengine ya vinywaji vikali.