Entertainment

RAPA CASANOVA AKABILIWA NA KOSA LA MAUJI

RAPA CASANOVA AKABILIWA NA KOSA LA MAUJI

Mwishoni mwa mwaka 2020 Rapa Casanova alikamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na genge la kihalifu liitwalo, Untouchable Gorilla Stone Nation, ambapo shirika la kijasusi nchini Marekani (FBI) lilitoa taarifa kupitia Twitter, taarifa ambayo ilikuwa ikiueleza umma kuwa inawashikilia member 17 wa genge hilo kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu, mauaji, dawa za kulevya na makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Casanova pamoja na genge hilo la kihalifu wanatajwa kuwa walihusika katika mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 15 huko Poughkeepsie, sasa rapa huyo ameshtakiwa kwa kosa la kujaribu kufanya mauaji.

Tukio hilo la kujaribu kufanya mauaji linaripotiwa kuwa lilitokea oktoba 24, mwaka wa 2020 mjini Miami Club alipogombana na mwanachama wa genge hasimu na kumshambulia kwa risasi tumboni.

Kwa mujibu wa ofisi ya mwanasheria mkuu mjini New York, Casanova pamoja na wenzake wakikutwa na hatia basi watakutana na kifungo cha maisha gerezani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *