Rapper Kanambo Dede ametimiza hatua muhimu katika maisha yake baada ya kukamilisha rasmi masomo yake ya sekondari.
Taarifa za kuhitimu kwake zimethibitishwa na msanii na mkurugenzi wa Kaka Empire, King Kaka, ambaye ameposti kipande cha video akiwa na Kanambo na kusisitiza kuwa mashabiki wajiandae kupokea muziki mzuri kutoka kwake.
King Kaka ameonyesha matumaini makubwa kwa nyota huyo chipukizi, akisema uamuzi wake wa kurudi shule na kutanguliza elimu ni jambo la kupongezwa.
Kanambo alirejea shuleni kupitia msaada na usimamizi wa Kaka Empire baada ya kupambana na umasikini na changamoto za ujauzito wa mapema.