
Rapa Kanye West ameripotiwa kutoonekana kwa wiki kadhaa na hata kwenye mawasiliano yake hapatikani.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizodakwa na Radaronline.com, meneja wake wa zamani, Thomas St. John amenukuliwa akisema kuwa amepata shida ya kumtafuta rapa huyo kwa kipindi cha wiki mbili sasa .
Kwa mujibu wa mtando wa TMZ, vyanzo vya karibu na familia ya Kanye West vimedai kuwa rapa huyo anasumbuliwa tena na matatizo ya akili, ambayo awali mwenyewe amewahi kuthibitishwa kuwa nayo.
Inadhaniwa kuwa matatizo hayo yanaweza yakawa ndio chanzo kilichopelekea kutoa kauli za utata katika siku za hivi karibuni.
Utakumbuka mwaka wa 2016, Kanye West alilazimika kusitisha show zake 21 baada ya kulazwa hospitalini kwa matatizo ya kiakili.