Entertainment

Rapa Khaligraph Jones,Amlilia Raila Odinga Baada ya Mazishi Bondo

Rapa Khaligraph Jones,Amlilia Raila Odinga Baada ya Mazishi Bondo

Rapa kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonyesha huzuni kubwa kufuatia mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Amolo Odinga yaliyofanyika leo nyumbani kwake eneo la Bondo, Kaunti ya Siaya.

Kupitia Insta stories yake, Rapa huyo amekiri kuumizwa sana na kifo cha kiongozi huyo, akisema kuwa tangu tukio hilo lifanyike amekuwa hana nguvu wala amani ya moyo. Ameongeza kuwa siku ya leo, ambayo ni ya mwisho ya kumpumzisha Odinga, inabeba uzito mkubwa kwa wale waliompenda na kumheshimu.

Kwa mujibu wake, amechoka kihisia kutokana na msiba huo na ameitumia siku hii kumtakia Baba pumziko la amani kwa heshima na upendo mkubwa.

Khaligraph Jones ni miongoni mwa maelfu ya Wakenya na mashabiki waliomuenzi Raila kama kiongozi mwenye maono, aliyepigania demokrasia na haki za wananchi kwa miongo kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *