Entertainment

Rapa King Kaka aachia rasmi Album yake mpya

Rapa King Kaka aachia rasmi Album yake mpya

Rapa King Kaka ameachia Album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Album aliyoipa jina la “2nd Life” ina jumla ya mikwaju 17 ya moto huku akiwa amewashirikisha wakali kama Wanavokali, Femi One, Iyaniii, Kanambo Dede,Solomon Mkubwa, Goodluck Gozbert na wengine wengi.

2nd Life ambayo ni Album ya sita kwa King Kaka, na tayari inapatikana kwenye mitandao yote ya ku-stream muziki duniani.

Ikumbukwe King Kaka ameachia Album kwa ajili ya kumrudishia Mwenyezi Mungu fadhila kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi duniani ikizingatiwa kuwa mwaka 2021 nusra ampoteze maisha yake baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana uliofanya kupoteza uzani wa kilo 33.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *