Entertainment

Rapa Sossun Awatetea Wasanii wa Kike Dhidi ya Ubaguzi wa Umri

Rapa Sossun Awatetea Wasanii wa Kike Dhidi ya Ubaguzi wa Umri

Rapper Sossun ameibuka kutetea wasanii wa kike nchini Kenya baada ya kuibuka kwa mijadala mitandaoni kufuatia wimbo mpya uliotolewa na Avril pamoja na Kendi.

Kupitia Instagramn yake, amesema kuwa vijana wa Gen Z wanapaswa kuacha kuwakosoa wasanii wa kizazi cha Gen X na Millennial kwa kigezo cha umri, akisisitiza kuwa hoja hiyo haina mashiko katika muziki.

Hitmaker huyo wa Sura ya Kazi, amebainisha pia kuwa kuna upendeleo katika tasnia ya muziki, kwani wasanii wa kiume kama Nyashinski na Nameless mara chache hukosolewa kuhusu umri wao, ilhali wenzao wa kike hufanyiwa mashambulizi ya maneno mitandaoni.

Kwa mtazamo wake, umri haupaswi kuwa kikwazo kwa wasanii wa kike kuendelea kuachia kazi mpya, kwani mashabiki wao pia wanakua pamoja nao na bado wataendelea kuwapa sapoti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *