Entertainment

Rapa Sylivia Ssaru atangaza kuja na Album mpya mwaka 2023

Rapa Sylivia Ssaru atangaza kuja na Album mpya mwaka 2023

Rapa wa kike nchini Ssaru ameweka wazi kuna huenda akaachia album ama EP mwanzo mwa mwaka 2023.

Kwenye mahojiano na Plug TV Ssaru amesema anaendelea na mchakato wa kuitayarisha mradi wake mpya ambao kwa mujibu wake amewashirikisha wasanii wa ndani na nje ya Kenya.

Mrembo ambaye mapema mwaka huu aliahidi kuachia EP mpya amewataka mashabiki kuwa na subira kipindi hiki yupo kwenye matayarisho ya mwisho ya kukamilisha kazi yake.

Lakini amenyosha maelezo kuhusu uhusiano wake na msanii Trio Mio kutokana na watu kumhusisha kutoka nae kimapenzi kwa kusema kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii huyo ambapo amedai ukaribu wao ni wa kikazi kama namna akifanya na wasanii wa kiume.

Hata hivyo amewataka watu kukoma kumhusisha kimapenzi na Trio Mio na badala yake wategemea makubwa kutoka kwao ikizingatiwa wana uhusiano mzuri kisanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *