Entertainment

RAPPER 50 CENT ATISHIA KUACHANA NA KAMPUNI YA STARZ

RAPPER 50 CENT ATISHIA KUACHANA NA KAMPUNI YA STARZ

Rapper kutoka Marekani 50 Cent ameingia kwenye headline mara baada ya kutishia kuondoka Starz, kampuni ambayo imechangia mafanikio makubwa ya series yake iitwayo ‘Power’.

50 Cent alisaini mkataba wa miaka minne na Starz tangu mwaka wa 2018 kwa kiasi cha shilling billion 17 za Kenya wa kufanya kazi ya kutengeneza series mbalimbali. Hata hivyo 50 cent hajaweka wazi chanzo cha kutaka kuachana na kampuni hiyo

Mkongwe huyo wa rap ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson III, kupitia ukurasa wake wa Instagram amewataka wafanyakazi wake chini ya kampuni yake ya G-Unit Film & Television kuanza kufungasha vitu vyao na kuondoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *