
Rapa kutoka nchini Marekani Kendrick Lamar ataikata kiu yako ya muziki muda wowote kuanzia sasa.
Jarida la BILLBOARD limeripoti kuna uwezekano mkubwa wa Rapa Kendrick lamar kuachia wimbo mpya kati ya Februali 2 au 11 Kabla hajapanda jukwaani katika tamasha la Super Bowl Halftime Show.
Tamasha hilo litawakutanisha maRapa kama Dr. Dre, Eminem, Snoop Dog, na linatarajiwa kufanyika Februari 13,mwaka huu wa 2022 Katika uwanja wa SoFi Stadium , California.
Utakumbuka August 20 mwaka wa 2021 Kendrick Lamar alidokeza ujio wa album yake mpya baada ya ukimya wa miaka 4, album ambayo aliitaja kuwa ya mwisho chini ya label ya Top Dog Entertainment, ambayo aliitumikia kwa miaka 17.