
Msanii nyota nchini Nyashinski ameahidi kujenga mji wake mpya nchini Kenya, mji ambao utatumika na mashabiki zake
Nyashinski ameyaweka wazi hayo Februari 13 mwaka huu kwenye moja ya performance yake iliyofanyika huko Two River Mall jijini Nairobi.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Properly” alienda mbali na kuwashauri wasanii wa muziki nchini watoa nyimbo zenye maudhui safi zitakazodumu kwa muda mrefu.
Hata hivyo amewaacha mashabiki zake na maswali mengi mara baada ya kufuta post zake zote kwenye mtandao wa instagram jambo ambalo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda rapa huyo ana matatizo ya kiakili huku wengine wakisema huenda ana mpango wa kuachia project yake mpya