
Ni rasmi sasa mkongwe wa Hiphop kutoka Marekani Snoop Dogg ndiye mmiliki wa lebo ya muziki ya Death Row Records.
Rapa huyo amenunua haki zote za lebo hiyo kongwe ambayo ilimtambulisha kwenye muziki miaka 30 iliyopita. Death Row Records ilikuwa inamilikiwa na kampuni ya MNRK Music Group.
Kwa mujibu wa taarifa kwa Waandishi wa habari ambayo imetolewa, Snoop Dogg ataiongoza Death Row Records kwa miaka ijayo akiwa kama mmiliki mpya.
Auncle Snoop alijiunga na lebo hiyo mwaka wa 1993 ambapo aliachia album yake ya kwanza, Doggy Style.
Death Row Records ilianzishwa na Dr. Dre, Suge Knight, The D.O.C. na Dick Griffey mwaka 1991 na imekuwa nyumba ya historia kwa kuwatoa wakali wa Hop Hop Marekani kutoka West Coast.