
Mkongwe wa muziki wa Hiphop nchini Marekani Snoop Dogg ameingia tena kwenye Headline Baada ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Akimporomoshea Matusi Dereva wa Uber Eats kwa kushindwa kumpeleka chakula.
Kwenye kipande cha video hiyo alichoshare kwenye Instagram page yake Snoop Dogg anaskika akimtusi Dereva huyo kwa hasira. “Chakula changu kiko wapi Umepata pesa zako zote Chakula kiko wapi.”
Kulingana na ripoti ya Complex, Dereva alifika na hakuwa na uhakika ni wapi pa kupeleka chakula hicho, kwa kuwa Auncle Snoop hakuwa mahali salama, ikizingatiwa kuwa alizidi kumuelekeza asogee Kwenye Geti Nyeusi aache chakula alicho muagiza.
Inaelezwa kuwa Dereva wa (Uber) Amemfungulia kesi Snoop Dogg kwa kumuhatarishia usalama wake kwa Kinachononekana kwenye video hiyo.
Kwa Mujibu wa Chanzo kilichopo karibu na Dereva uber kimemnukuu Dereva akisema “Ni picha yangu Hapo pia kuna jina langu la kwanza,..” Baada ya kuona video, imenipa wasiwasi, mwingi na ninahofia usalama wa familia yangu. Niliwasiliana na mteja Mara nyingi na nikafuata itifaki ya Ramani..Ila hakuwa sehemu salama” .Dereva, aitwaye Sayd, alisema.