Entertainment

Rayvanny Afichua Mpango wa Kufanya EP na Wasanii Chipukizi

Rayvanny Afichua Mpango wa Kufanya EP na Wasanii Chipukizi

Mwanamuziki nyota wa Tanzania, Rayvanny, ametangaza mpango mpya wa kuibua vipaji kwa kutengeneza EP maalum akiwashirikisha wasanii chipukizi kutoka mitaani.

Kupitia mitandao ya kijamii, Rayvanny amesema lengo ni kuwapa nafasi vijana wenye uwezo mkubwa lakini wasio na majukwaa ya kujitangaza. Ameongeza kuwa safari yake ya mafanikio ilisaidiwa na watu waliomuamini, hivyo hana budi kuwarudishia fadhila kwa kuinua kizazi kipya cha wasanii.

Msanii huyo wa ngoma ya Songi Songi, amewahimiza mashabiki kuendelea kupendekeza majina ya madogo wakali wanaowafahamu ili wapate nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia mradi huo mpya wa muziki.

Kauli yake imekuja mara baada ya mashabiki kupendekeza majina ya wasanii mbalimbali chipukizi alipotangaza nia ya kufanya kazi na kijana mmoja aliyeonyesha kipaji chake mwezi Juni mwaka huu kupitia mitandao ya kijamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *