
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny, amefunguka kuhusu maumivu aliyopitia kutokana na kile alichokiita usaliti kutoka kwa msanii mwenzake Mbosso.
Kwenye mahojiano na waadishi wa habari, Rayvanny amesema aliumizwa sana baada ya kusikia kuwa Mbosso alimsema vibaya kwa Diamond Platinumz wakati alipokuwa akiondoka kwenye lebo ya WCB Wasafi. Hitmaker huyo wa “Mama Tetema” amefafanua kuwa, licha ya tofauti zilizojitokeza, yeye ndiye aliyepigania Mbosso kusainiwa kwenye lebo hiyo.
Lakini pia amekiri kwamba yeye ndiye aliyemuunganisha Baba Levo na Diamond, jambo lililomsaidia kupata nafasi ya ajira ndani ya WCB. Kwa mujibu wa Bosi huyo wa Next Level, jambo la kushangaza ni kwamba licha ya mchango wake mkubwa kwa wasanii hao wawili, wamekuwa wakimzungumzia vibaya badala ya kumshukuru.