Entertainment

Rayvanny akiri kukua kisanaa tangu aondoke WCB

Rayvanny akiri kukua kisanaa tangu aondoke WCB

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Rayvanny amesema tangu aondoke kwenye Label ya WCB amejihisi kukua Kimuziki na kwa sasa anawaza mambo makubwa zaidi.

Akizungumza na mtandao wa Habari Leo, amesema changamoto anazokutana nazo pamoja na ushindani uliopo kwenye game ya bongo fleva, vimemkomaza zaidi.

β€œUkweli sijutii maamuzi yangu, zaidi napambana ili niweze kuwa mkubwa zaidi, sababu huku kila kitu wakuulizwa ni Mimi na sababu ndio Boss mkubwa ninayehusika na mambo yote ikiwemo kulipa wasanii na mengineyo.” amesema Rayvanny.

Aidha amesema kwa jinsi anavyofanya vizuri katika game hiyo, anaamini mpaka kufikia mwaka ujao atakuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini na wenye wafuasi wengi kuliko ilivyo hivi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *