Entertainment

RAYVANNY KUTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA MTV EUROPE MUSIC AWARDS 2021

RAYVANNY KUTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA MTV EUROPE MUSIC AWARDS 2021

Mkurugenzi wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ametajawa kuwa msanii pekee atayetumbuiza kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards ambazo kwa mwaka huu 2021 zitatolewa huko nchini Hungury.

Kwa mara ya kwanza Rayvanny atatumbuiza kwenye jukwaa hilo la tuzo za kimataifa akiwa na msanii kutoka nchini Columbia aitwaye maluma ambaye amemshirikisha Rayvanny kwenye wimbo wao uitwao Mama Tetema ambao kwa mara ya kwanza utasikika kwenye tuzo hizo za mtv Europe music awards.

Taarifa hizo zimetolewa na mtv Europe music awards  kupitia ukurasa wao  Twitter.

Maluma ni moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Latin America akiwa na zaidi ya subscribers Milioni 27 kwenye mtandao wa YouTube, na Followers zaidi ya Milioni 50 kwenye mtandao wa Instagram.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika November 14,mwaka wa 2021 huko nchini Hungury huku Afrika Mashariki tukiwa tunawakilishwa na diamond platnumz ambaye ametajwa kwenye kipengele cha Best African Act

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *