
Staa wa muziki wa BongoFleva Rayvanny ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bosi huyo wa Next Level Music amethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kuwa mwaka huu 2023 ataachia EP ya ‘Flowers III’.
‘Flowers III’ itaifuata EP yake ya ‘Flowers II’ aliyoiachia Februari 10, mwaka 2022 iliyokuwa imebeba nyimbo tisa huku ikiwa na kolabo sita tuu za wasanii kama Marioo, Zuchu na wengine wengi.
Kama wewe ni mmoja kati ya watu waliofurahia mtiririko wa EP za ‘Flowers’ kutoka kwa Rayvanny basi yaandae masikio yako kwa ajili ya muendelezo wa EP hizo.