Entertainment

Remix ya “Pawa” Yamletea Nyota Ndogo Zawadi ya KSh100,000 Kutoka kwa Khaligraph Jones

Remix ya “Pawa” Yamletea Nyota Ndogo Zawadi ya KSh100,000 Kutoka kwa Khaligraph Jones

Mwanamuziki wa Pwani, Nyota Ndogo, amejipatia zawadi ya shilingi laki moja kutoka kwa rapa Khaligraph Jones, hatua inayohusishwa moja kwa moja na kampeni yake ya hivi karibuni ya kumtetea Papa Jones aingizwe kwenye remix ya wimbo “Pawa” wa Mbosso.

Nyota Ndogo amefichua kupitia Instagram kuwa alishtuka alipokea ujumbe wa malipo (M-PESA) kutoka kwa Khaligraph, akieleza kuwa rapa huyo alimwambia zawadi hiyo ilikuwa ni ishara ya kumshukuru kwa kusimama upande wake kwenye mjadala wa remix hiyo.

Wiki kadhaa zilizopita, Nyota Ndogo alitumia mitandao ya kijamii kushinikiza wasanii na mashabiki kuona umuhimu wa Khaligraph kushirikishwa katika remix ya Pawa. Alisisitiza kuwa iwapo rapa huyo angepewa nafasi, remix ya Mbosso ingezidi kupata nguvu na mvuto mkubwa katika soko la muziki wa Afrika Mashariki.

Kitendo cha Khaligraph kimepongezwa na mashabiki mitandaoni, wengi wakikitafsiri kama heshima kubwa kwa msanii huyo wa Pwani na pia kuthibitisha jinsi rapa huyo anavyoweza kuthamini wale wanaomuunga mkono.

Kwa sasa, bado haijathibitishwa rasmi iwapo Khaligraph atashirikishwa kwenye remix ya Mbosso, lakini tukio hili limezua mjadala mpana kuhusu ushirikiano wa wasanii wa Tanzania na Kenya, na jinsi sapoti ya wasanii wenzao inaweza kubadilisha mwelekeo wa muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *