Entertainment

Rickman Manrick adokeza ujio wa EP yake mpya

Rickman Manrick adokeza ujio wa EP yake mpya

Mwanamuziki Rickman Manrick ametangaza ujio wa Extended Play (EP) ambayo ana mpango wa kuachia mapema mwaka huu.

Rickman anasema EP yake itaingia sokoni mwezi Februari 2023 ingawa bado hajaweka wazi jina na idadi ya nyimbo ambayo itapatikana kwenye EP hiyo.

Msanii huyo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea nyimbo kali kutoka kwa EP yake hiyo huku akiongeza kuwa anaamini itapeleka tasnia ya muziki nchini Uganda kimataifa zaidi.

“Niliacha freestyle iitwayo ‘Luga Pandemic’ juzi. Nina EP ambayo inakuja hivi karibuni. Nitaiacha mwezi Februari. Kwa hivyo, ninyi watu wangu kaeni tayari kwa ajili ya muziki mzuri,” Alisema Rickman.

Ikumbukwe baadhi ya mashabiki wanaamini kwamba kama Rickman angesimama na muziki wa rap, angekuwa msanii bora zaidi nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *