
Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Ringtone Apoko ameibuka na kuwaomba Wakenya msamaha mara baada ya kuzozana na DJ MO kwenye uzinduzi wa album msanii mwenzake Size 8 wikiendi hii iliyopita.
Katika mkao na wanahabari Ringtone amekiri kutopendezwa na kitendo cha kuzua vurugu kwenye shughuli za watu kwa kusema kwamba anajuta kuwaibisha mashabiki zake kwa kujihusisha na vitendo vya kiuhuni ambavyo vinakwenda kinyume na mafunzo ya kikristo.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sisi Ndio Tuko” ameahapa kutorudia tena ishu ya kuzua vurugu sehemu yeyote ile kwani jambo hilo imeleta picha mbaya kwa jamii ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao watu wamekuwa wakiheshimika kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini.
Utakumbuka Februari 13 mwaka huu kwenye uzinduzi wa album ya mwanamuziki Size 8, Ringtone alifurushwa na waandaji wa hafla hiyo baada ya kutaka kujiunga na wahubiri stejini kwa lazima kuibariki album ya Size 8.