
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Ringtone Apoko amezua mjadala mzito mtandaoni mara baada ya kutoa ushauri kwa wanaume ambao wapo mbioni kuingia kwenye ndoa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone ame-posti picha ya pamoja ya William Ruto, Uhuru Kenyatta na wake zao na kusindikiza na caption inayowataka wanaume kuwaoa wanawake ambao ni wafupi kwa kimo kwa sababu wana nyota ya mafanikio kwenye maisha.
Hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” ameenda mbali zaidi na kuwaonya wanaume kutowachumbia wanawake warefu, akiwataja ni vizingiti kwenye masuala ya mafanikio.
“PLEASE ALL MEN MARRY SHORT WOMEN IF U IS WANT TO MAKE IT AT YOUR LIFE PLEASE LEFT TALL WOMEN ALONE TALL WOMEN WILL STOLEN YOUR STAR ”, Ameandika.
Kauli yake imeibua hisia miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wametilia shaka uwezo wa kufikiria wa msanii huyo huku wengine wakimtaka arudi darasani kwa ajili ya kupata mafunzo fasaha ya lugha ya kiingereza.