Entertainment

RINGTONE APOKO AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUINGIA KWENYE NDOA

RINGTONE APOKO AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUINGIA KWENYE NDOA

Inaonekana upweke unazidi kumtesa msanii wa nyimbo za Injili nchini Ringtone Apoko mara baada ya kuweka wazi matamanio yake ya kuingia kwenye ndoa.

Kupitia Instagram Page yake msanii huyo ameibuka na kutangaza hadharani kwamba anataka mke kwa sasa, maana kifedha anazidi kuwa tajiri tu.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sisi Ndio Tuko” ameenda mbali zaidi na kuwataka mashabiki zake wamsaidie kumtafutia mke wa ndoto yake.

Hata hivyo post hiyo haikuwa na uhai wa muda mrefu kwani Ringtone aliufuta ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwaacha mashabiki na maswali mengi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ringtone Apoko kutangaza wazi kuwa anataka kuoa, mwezi Juni mwaka wa 2019 pia alieleza hisia zake kupitia wimbo wake uitwao “Nafuta Bibi.” ambao una zaidi ya views millioni moja kwenye mtandao wa Youtube.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *