
Mtayarishaji wa muziki wa Bongofleva Yogo Beats ambaye amehusika kwa kiasi kikubwa kutengeneza album ya mwanamuziki Ali Kiba “Only One King” ameweka wazi kuwa album hiyo imefikisha zaidi ya streams million 175 katika digital platforms zote za kuuza na kusikiliza kazi za muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram yake Yogo ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki katika tuzo za Tanzania Music Awards , ameeleza kuwa album hiyo ina jumla ya streams million 36 katika mtandao wa Boomplay huku ikiwa na streams million 16 katika mtandao wa wa Audiomack.
Ikumbukwe album hiyo ambayo ilitoka mwezi Oktoba mwaka jana ikiwa na jumla ya nyimbo 16 za moto, ni album ya tatu kwa alikiba, baada ya Cinderella (2007) na AliK4Real (2009).