
DJ wa Diamond Platinumz ambaye pia ni Kaka wa bosi huyo wa WCB Romy Jons amewataka watu wapendane hata kama mtu hana mbele wala nyuma
Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa Romy Jons amewataka watu wathaminiane ujumbe uliomaanisha kuwa hakuna aijuaye kesho yako au yake.
“Kuna baadhi ya ndugu/marafiki walimdharau sana na kumkebehi mdogo wangu nasibu, hakuna alieamini katika ndoto yake, leo ndio hao mstari wa mbele kuomba msaada, tupendane na kuthaminiana hata kama hatuna mbele wala nyuma”. Ameandika kwenye Istagram yake.
Hii inakuja mara baada ya watu waliomdharau mdogo wake Diamond Platnumz kwa kutoamini katika ndoto yake kipindi cha nyuma lakini leo wamekuwa mstari wa mbele kwenye suala la kumuomba msaada.