Rapper kutoka Tanzania Roma Mkatoliki amemtambulisha mtoto wake mwingine ambaye bado hajaweka wazi kuhusu utambulisho wake.
Roma ambaye amekuwa akiisha nchini Marekani kwa miaka kadhaa sasa, amechapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha akiwa na gari maalum ya kubebea watoto na kuambatanisha na ujumbe unaosomeka “Kitanda Hakizai Haramu”
Hata hivyo picha hiyo imewaacha wafuasi wake na maswali mengi huku wakihoji Roma amezaa na nani wakati mke wake wa ndoa yupo nchini kwao Tanzania.
Wengi wametafsiri kitendo hicho kama Roma atakuwa amezaa na mwanamke mwingine na sio mke wake Mama Ivan.