Entertainment

Ronald Alimpa akiri kuacha kutumia dawa za kulevya

Ronald Alimpa akiri kuacha kutumia dawa za kulevya

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ronald Alimpa amekiri kuwa amekuwa akitumia mihadarati kama wasanii wengine duniani.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni anasema wakati huo alikuwa akivuta bangi na hakuna mtu ambaye angemzuia kufanya chochote alichotaka kwani hakuwa amekumbana na madhara ya kutumia dawa za kulevya.

Hata hivyo, Ronald Alimpa amethibitisha kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya kulazwa hospitalini kufuatia kunusurika kwenye ajali mbaya ya barabarani.

Msanii huyo anasema maumivu aliyokuwa nayo wakati wa operesheni yalikuwa makali, hivyo madaktari walimshauri aachane na dawa za kulevya kwani huenda ingeathiri maisha yake siku za mbeleni.

Katika hatua nyingine Alimpa amefichua ujio wa wimbo wake mpya uitwao  “Onyenyangamu” ambao utaingia sokoni hivi karibuni.

Anasema wimbo wake mpya unauachia kwa ajili ya kusherehekea uhai wake na pia kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha kwani nusra aage dunia alipohusika kwenye ajali mbaya ya barabarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *