
Baada ya Malkia wa muziki wa injili Tanzania Mtumishi wa Mungu Rose Muhando kufunga mwaka 2022 kibabe kwa kutoa Album yake iitwayo Secret Agenda ambayo hadi hivi sasa imepata mapokezi makubwa mnoo kwa wadau na wapenzi wa muziki wa injili.
Sasa mwaka 2023 pia Mungu ameendelea kuwa upande wake kwa kufungua mwaka kwa kupata Tuzo mbili kubwa na za kimataifa zinazoitwa RSW AWARDS Tuzo hizo zinazotolewa huko Australia.
Rose Muhando ameshinda Tuzo mbili kupitia kipengele cha African Female Gospel Vocalist pamoja na kipengele cha African Gospel collaboration, Tuzo hizi zimepangwa kutolewa huko Australia in Adelaide, South AUSTRALIA on 18th Februari 2023.