
Mahakama kuu jijini Abuja nchini Nigeria imetoa rasmi talaka ya waliokuwa mume na mke, Paul Okye a.k.a Rude Boy na Anita Okoye Desemba 20,mwaka 2022, ikiwa ni baada ya mwaka kupita tangu shauri hilo lifikishwe mahakamani na Anita Okoye, Agosti mwaka 2021.
Anita Okoye alifungua shauri la talaka kwa kile alichodai kuchoshwa na usaliti wa mumewe ambao amekuwa akiufanya mara nyingi kwa kutoka kimapenzi na msaidizi wao wa kazi za nyumbani, lakini pia amekuwa si baba muwajibikaji kwa watoto wao watatu, hajali chochote kuhusiana na familia. Kwenye shauri hilo la talaka pia kuliambatanishwa madai ya pesa ya malezi kwa kila mwezi, kiasi cha dollar za kimarekani elfu 20 zaidi ya milioni 46.6 za kitanzania.
Lakini pia Anita ametaka kurudishiwa pesa kiasi cha Naira milioni 10, zaidi ya milioni 2.8 za Kenya ambazo alimpa mumewe kuongeza ardhi kwaajili ya kujenga Shopping Mall chini ya kampuni yao ya TannkCo Premises, lakini pesa hizo ziliishia kutafunwa na mumewe huyo bila kufanyiwa lolote.
Safari ya mahusiano yao ilianza mwaka 2004 wakiwa Chuo, na baada ya miaka 10, (2014) wawili hao walifunga ndoa na kujaaliwa watoto 3