Entertainment

S2kizzy Ajiita Profesa wa Muziki, Awahimiza Beatmakers Kujiamini Zaidi

S2kizzy Ajiita Profesa wa Muziki, Awahimiza  Beatmakers Kujiamini Zaidi

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania, S2kizzy maarufu Zombie, ameweka wazi mtazamo wake kuhusu nafasi ya beatmaker katika tasnia ya muziki.

Akipiga stori na The Throne, Zombie anasema hakuna haja mtu yeyote kujisikia vibaya akiitwa beatmaker kwa sababu hiyo ndiyo nguzo muhimu inayoshikilia mchakato mzima wa utayarishaji muziki.

Kwa maelezo yake, kutengeneza beat ndiko kunakoipa ngoma uhai kabla ya hatua nyingine za uzalishaji kuingia. Hata hivyo, anasisitiza kuwa safari yake ya kimuziki imemfikisha mbali zaidi ya hatua hiyo, na sasa anajitazama kama profesa wa muziki kutokana na uwezo wake mpana unaojumuisha kuunda beat, kufanya production, kutoa mwongozo na kupanga mashairi.

S2kizzy, ambaye amefanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki na kimataifa akiwemo Diamond Platnumz, Rayvanny na Harmonize, amekuwa akihusishwa na mageuzi makubwa kwenye sauti ya Bongofleva na kuisukuma kuvuka mipaka ya kanda.

Wachambuzi wa muziki wanasema matamshi yake yanaonyesha namna tasnia inavyoendelea kukua na kuhitaji wataalamu wenye ujuzi mpana zaidi ya kutengeneza beat pekee, kwani muziki wa kisasa unahitaji ubunifu, usimamizi wa kiufundi na mtazamo wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *