Entertainment

S2kizzy Amporomoshea Matusi Hussen Machozi

S2kizzy Amporomoshea Matusi Hussen Machozi

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, S2kizzy, ameimtolea maneno makali mwanamuziki Hussen Machozi, akimuita mpumbavu.

Akipiga stori na East Africa Radio, mtayarishaji huyo amesema hana sababu ya kushirikiana naye kimuziki ikizingatiwa kuwa nyimbo zake zimepitwa na wakati.

S2kizzy anayejulikana kwa jina la utani Zombie amemchana vikali Machozi na kutamka wazi kuwa hamheshimu huku akimshauri msanii huyo kutafuta njia nyingine za kuendeleza muziki wake.

Kauli ya S2kizzy imeibuka kufuatia madai ya Hussen Machozi, aliyelalamika kuwa mtayarishaji huyo hajawahi pokea simu zake licha ya kujitambulisha kwake mapema. Hussen alienda mbali zaidi na kuhoji kuwa juhudi zake za kuwasiliana na S2kizzy zimekuwa zikigonga mwamba, jambo lililomfanya kulalamikia kutothaminiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *