Entertainment

S2Kizzy Atoa Msaada kwa Prodyuza Bakteria Aliyepooza Baada ya Kushambuliwa

S2Kizzy Atoa Msaada kwa Prodyuza Bakteria Aliyepooza Baada ya Kushambuliwa

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania, S2Kizzy maarufu Zombie, ameonyesha moyo wa utu baada ya kumtembelea na kumpa msaada prodyuza mwenzake aitwaye Bakteria, ambaye kwa miaka miwili sasa amekuwa akikabiliwa na changamoto kubwa ya kiafya.

Katika ziara yake, S2Kizzy alimpelekea msaada wa vyakula na mahitaji ya nyumbani, huku akisisitiza kuwa Bakteria alikuwa tegemeo kubwa kwa familia yake kupitia kazi za muziki, lakini sasa hali ngumu imemlazimisha kusimama. Ameongeza kuwa ni muhimu jamii iungane na kusimama pamoja na wale wanaopitia changamoto.

Zombie ametoa wito kwa mashabiki na watu wenye nia njema kushirikiana na kusaidia familia hiyo kupitia namba 0714 315 680.

Bakteria alipata matatizo ya kupooza na kushindwa kutembea kufuatia shambulio la vibaka karibu na studio yake mjini Tanga, jambo lililosimamisha kabisa ndoto zake za muziki. Kwa sasa, Bakteria anaishi na mama yake mzazi ambaye pia anakabiliwa na matatizo ya kiafya, hali inayoongeza ugumu wa maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *