
Prodyuza wa muziki kutoka Tanzania, S2kizzy, amewashauri maprodyuza wenzake kutoogopa kufanya aina yoyote ya muziki kwa kuhofia maneno ya watu.
Kwa mujibu wa S2kizzy, muziki ni sanaa ya burudani na furaha, hivyo kila prodyuza ana nafasi ya kujaribu mitindo na miondoko mbalimbali ili kuleta furaha na burudani kwa jamii.
S2kizzy, ambaye amehusishwa na kutengeneza hit singles nyingi za wasanii wakubwa Afrika Mashariki, amesisitiza kuwa ubunifu na kujiamini katika kazi ndiyo msingi wa mafanikio katika tasnia ya muziki ambayo imejaa ushindani mkubwa.
Ujumbe huu umetafsiriwa kama motisha kwa vijana wengi wanaojitahidi kuingia kwenye muziki lakini hukumbwa na hofu ya mitazamo ya watu